Misungwi: Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mh. Juma Sweda akikagua mojawapo ya soko la madini ya Dhahabu linalojengwa Misungwi katika eneo la Shilalo ambapo kuna shughuli za uchimbaji mdogo hzinazoendelea kwa wachimbaji wadogo kuchimba Dhahabu na kuuza ili kujipatia fedha ya kujikimu katika maisha yao ya kila siku. Mkuu wa wilaya amewaomba wachimbaji hao kutumia soko hilo wakati wa kuuza Dhahabu yao ili kujipatia kipato na kuifanya serikali iweze kukuza uchumi wake kutokana na Dhahabu inayopatikana katika maeneo yetu, kutokana na kodi itakayopatikana kwa mujibu wa sheria za madini. Uanzishwaji wa masoko haya ni kuepusha uuzwaji holela wa Dhahabu unaoikosesha serikali kipato. Wachimbaji wa madini wadogo katika eneo la Shilalo, tutumieni soko hili kwa kuuza rasilimali yetu adimu ya Dhahabu ili kuinua uchumi wa Shilalo, wilaya yetu ya Misungwi na taifa letu kwa ujumla. Mipango na mikakati ya awamu ya tano ni endelevu kwa kuhakikisha inainua uchumi na kipato cha kila mwananchi (Mtanzania) kwa kumjengea mazingira bora ya uzalishaji Mali.
Pichani; ni baadhi ya wachimbaji wadodo katika machimbo ya Dhahabu Shilalo wakiwasikiliza viongozi kwa makini juu ya utumiaji wa masoko ya madini wakati wa kuuza Dhahabu wanayoipata kutokana na shughuli yao ya uchimbaji.
Pichani hapo juu; ni mojawapo ya mashine ya kusaga mawe ya Dhahabu alimaarufu hujulikana kwa jina la Karasha.
Pichani; ni sehemu mojawapo inayotumika kwa shughuli ya uoshaji wa Dhahabu baada ya mawe ya Dhahabu kusagwa, alimaarufu hujulikana kama sehemu ya kuchenjulia Dhahabu.
No comments:
Post a Comment