Friday, August 23, 2019

Kampuni ya Nebrix Ltd ni Mzabuni wa Kuigwa katika Sekta ya Elimu Misungwi"


  1. Misungwi; Afisa Masoko wa Kampuni ya Nebrix Ltd, Mwanza, Ayubu Robert  Ng”hwelo amekabidhi msaada wa Vitabu  50 (masomo mbalimbali), Tufe 1, Dustbin 5 za kuhifadhia taka laini, Heart Model 1, Charts 20, First Aid Kit 1, na Skeleton Model 1 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya (w) Misungwi Bw, Kisena Mabuba kwa lengo la kuvipeleka katika shule za Sekondari zilizoko Misungwi ili kuleta ufanisi katika tendo zima la Ufundishaji na Ujifunzaji. Vifaa vilivyotolewa vina thamani ya Tsh. 4,300,000/= (milioni nne na laki tatu tu) 

    Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya (w) Misungwi Ndg, Kisena Mabuba ameishukuru kampuni hiyo kwa kuona ni vyema kusaidia shule za sekondari kwa vifaa mbalimbali walivyotoa, hii inaonyesha wanajali sana elimu kwa maana wameweza kutumia faida waliyoipata kusaidia kuinua elimu katika wilaya yetu ya Misungwi. Hii ni moja ya kujivunia wazabuni ikiwa wanarejesha faida katika shughuli za maendeleo (returns) na kwa kufanya hivyo tutakuwa wazalendo kwa taifa letu.

    Kitendo hiki cha kujitoa kusaidia kuinua elimu  kwa vifaa vilivyotolewa kimemfurahisha Bi, Dianah Kuboja Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Misungwi, na amesema vifaa vilivyotolewa vitapelekwa katika  shule mbili za sekondari ambazo zimeanza hivi karibuni ili kukabiliana na upungufu uliopo ambazo ni shule ya sekondari Mamaye na J. Magufuli.


    Shukurani za pekee kwa Kampuni ya Nebrix Ltd kutambua umuhimu wa Elimu, na kuweza kutoa mchango wao ili kuinua kiwango cha ufaulu katika sekta ya elimu ngazi ya sekondari Misungwi.

    0

    Ongeza maoni



    Inapakia

    No comments:

    Post a Comment